Ujumbe wa Mheshimiwa Mbunge El-Hadj Hussein RADJABU baada ya kutoka jela kuu ya Mpimba tarehe 1 Machi 2015
Tarehe 26 machi 15

UJUMBE WA MHESHIMIWA MBUNGE EL-HADJ HUSSEIN RADJABU BAADA YA KUTOKA JELA KUU YA MPIMBA TAREHE 1 MACHI 2015
 • Waheshimiwa Mabibi na Mabwana Mabalozi,
 • Wawakilishi wa mashirika ya kimataifa na wale wa mashirika yasiyokuwa ya kiserikali nchini Burundi,
 • Ndugu wananchi,
 • Ndugu wanachama wa CNDD-FDD na UPD-Zigamibanga,

Kwa furaha isiyo na kifani, kutoka mahali nilipo hifadhiwa ,naomba kwa heshma na taadhima nitowe salamu zangu za umoja na amani.

Nyote mnafahamu kwamba tumelazimishwa kutoka nchini baada ya miaka nane ya upangaji usiyo wa khiari,unyanyasaji na udhalishaji katika gereza kuu la Mpimba.

Awali ya yote napenda kumshukuru Mwenyezi Mungu mwingi wa rehma na huruma, aliyetulinda na kutuongoza katika kipindi cha miaka nane ya matatizo magumu aliyotukumba,mimi na wenzangu, katika gereza kuu la Mpimba na magereza mengine nchini; hali iliyopelekea wengine kuikimbia nchi.

Naomba kutumia nafasi hii kutowa shukrani zetu za dhati kwa warundi wote; hususani wanasiasa, viongozi wa dini, viongozi wa mashirika ya kitaifa na kimataifa ya kutetea haki za binadamu,mabalozi wanaowakilisha nchi zao hapa Burundi, mashirika ya kisiasa na kiuchumi ya kanda ya ziwa;pasipo kusahawu vyombo vya habari walivyo tuunga mkono na kuwa karibu yetu katika nyakati ngumu zilizotukumba mimi na wengine warundi wengi.

Shukrani zetu za dhati twazielekeza pia kwa ndungu na jamaa wote ambao kwa kadri ya uwezo wawo waliendelea kuwa karibu nasi, kwa wabunge wenzangu wa CNDD-FDD waliofukuzwa bungeni kinyume na sheria na bila kusahau Shirikisho la Mambunge ulimwenguni ambao kwa moyo mwema walitusikiliza vema wakati wote tulipokuwa tunawaelezea matatizo yetu. Tunatambuwa kwamba wakati wowote tuta pohitaji msaada wao tutaupata kwa haraka.

 • Ndugu wanachama wa CNDD-FDD
 • Ndugu wanachama wa UPD-Zigamibanga
 • Mabibi na Mabwana,
Usiku wa tarehe mosi machi mwaka 2015 hautasahwlika maishani mwangu na yenu pia. Siku ambayo Mwenyezi Mungu alitutowa kwenye minyororo ya adui zetu. Shughuli hiyo ya aina yake isingefanikiwa bila ushirikiano,ujasiri na ari thabiti ya wale wote miongoni mwenu walio chukuwa uamuzi wakuweka kikomo wa vitendo vibovu vya siasa za aibu na upumbavu ambayo dhamira yake ilikuwa ni kututelekeza gerezani daima. Kitendo hicho cha ushuja ni ishara ya kutofanikisha malengo yao ya utawala wa kibeberu wa Bujumbura. Ni dhahiri kwamba mtu mmoja ao watu wachache wasingeweza kufikia hayo mafanikio.

Kwa hali yoyote ile, kututenga na wafungwa wengine na kutokubali kutuachia kwa dhamana; ni dalili ya kutokua hodari , hisia hafifu za watawala na haswa kukiri ku mong’omnyoka kwa utawala badala ya kufikiria mikakati ya kupambana na hali ilivyo.

Dhamira yetu siyo kulipiza ao kuweka kisasi bali ni kuondowa kisasi kwa sababu kiongozi bora ni yule anaye waombea mema hata wapinzani wake. Ni tofauti na yaliyo tamkwa na waziri mmoja wa serilikali akisema kwamba tuwakosefu wa nidhamu wakati sisi na watu wa amani.

Baadhi ya wanasiasa waliyo madarakani waigiza kwamba wamuamini Mungu. Na wakati huyo huyo wana angamiza maisha ya binadamu wenzao. Kufunga raia wema bila kujuta wala huzuni, kujenga mifumo tofauti ya mauaji, kudhalilisha binadamu wenzao, kuamini kwamba unamilika maisha ya viumbe wote; hizo ni dalili kamili za ukafiri na ishara za mfamaji.

Natumia nafasi yangu ya mwenyekiti halali wa chama CNDD-FDD na mzalendo aliye kuwa mpiganaji nabado anashirikiana nanyi katika mpambano wa kurejesha taifa linatawaliwa kwenye misingi ya haki na ushindi wa demokrasia;kuwaletea ujumbe wa amani,maridhiano,umoja na mshikamano.

Hata kama mapambano haya ni magumu,ila ni matakatifu. Kama mnavyofahamu mpambano huyo wa warundi ulipitia kwenye mchakato mrefu. Ni baada ya vita ya wenye kwa wenyewe iliyo sababisha umwagaji wa damu nyingi ,vita ambayo tulipoteza wazazi na ndungu zetu ; tulipata amani na uhuru.

Uhakika ni kwamba safari bado ni ndefu ila ukweli ni kwamba historia yenyewe inasonga mbele. Demokrasia ni mfumo wa maisha siyo maneno. Duniani kote utawala ni wa raia.Watu wachache wanaweza kufanikiwa kuchukua madaraka na kunyanyasa raia ila hatima yake ya raia watashinda. Kama tumesema hapo awali ;amani , demokrasiya na maendeleo ya nchi ni mchakato mrefu unaimarika baada ya vizazi kadha.Hayo ndiyo tuliwafundisha manachama wetu.

Kwa bahati mbaya,adui zetu na walafi wa madaraka waliungama na kupotosha raia kwa lengo la kuhodhi chama chetu CNDD-FDD na mshirika wetu UPD-ZIGAMIBANGA. Walifanikiwa kukitumia kwa kutekeleza maovu yao na mipango yao ya kusambaratisha mfumo wa vyama vingi.

 • Ndungu wananchi,
 • Ndungu wanachama wa CNDD-FDD,
 • Ndungu wanachama wa UPD-ZIGAMIBANGA,
 • Mabibi na Mabwana ,
Tukichunguza ya uongozi wa nchi, mtaafikiana na mimi kwamba toka 2007 utawala mbovu, ubadhirifu , uporaji wa mali ya umma na maovu mengine yaliyo na athari hasi kwa warundi vilikoma siku bada ya siku.

Kuhusu ubadhilifu wa mali ya umma kumedhihirika rushwa katika hatua za ubinafsishaji na uuzaji wa mali ya umma. Kumeonekana rushwa pia katika uchimbaji haramu wa madini na mengine mengi. Hayo yote yakifunikwa na utoaji zabuni kinyume na sheria.

Kuhusiana na suala la usalama na uhuru wa raia kwa ujumla vilihatarishwa na waliokua wakitakiwa kuvilinda. Toka 2007 raia wamekosa amani kutokana na kufungwa kiholela pasipo kuwa na sabau za msingi, na tabia ya unyanyasaji inayo fanywa na mapolisi wa idara ya upelelezi. Kufungwa kwa watetezi wa haki wa binadamu pamoja na waandishi wa habari kama Jean Claude KAVUMBAGU, Hassan RUVAKUKI, Pierre Claver MBONIMPA, Bob RUGURIKA na wengine wengi ni mmoja ya mifano inayodhihirisha unyanyasaji huo.

Zaidi ya hapo ripoti mbaya ya usalama na haki za binadamu zinaipatia sura mbaya nchi yetu. Hizo nazo ni kama ripoti za ukiukaji wa sharia, ripoti za maiti zilizokutwa ndani ya ziwa Rweru, ripoti ya uvamizi wa Cibitoke uliofanywa na watu waliobebelea silaha.

Kuhusiana na mahusiano baina ya nchi ya Rwanda na Burundi, inatakiwa kuteuliwa kamati aliyoafikiwa na pande zote itakayoweka bayana maeneo yenye matatizo ya mipaka.

Sehemu ambazo matatizo haya yamejitokeza zaidi ni Cibitoke, Kirundo, Muyinga na Ngozi. Tuwakumbushe kwamba imeshafanyika mikutano mingi yenye lengo la kutafutia ufumbuzi tatizo hilo la mipaka. Tunawajulisha kwamba paliwahi kutokea matatizo katika mlima Sabanegwa uliyo katika wilaya ya Mwumba mkoani Ngozi baada ya mto Kanyaru kutupa mkondo wake. Matatizo kama haya yalijitokeza tena mkoani Muyinga wilayani Giteranyi tarafani Ruzo.

Hivi sasa ni wakati muafaka kwa mahusika wa masuala ya kidiplomasia nchini Burundi kulivalia njuga tatizo hili lenye zaidi ya miaka 50 ambalo limekua likijitokeza mara kwa mara na linaweza likaleta uhasama baina ya mahusiano ya nchi hizi mbili.

Suala lingine ni kwamba serikali ya Nkurunziza na sanasana idara ya upelelezi vinashutumiwa mauaji ya kikatili yaliyofanyiwa watawa wa kitaliano katika parokia ya Kamenge. Hivyo pia vinaweza vikaathiri mahusiano baina ya nchi ya Burundi na Umoja wa Ulaya na hasa makao makuu ya kanisa katoliki Vatican. Hili tatizo lazima liwekwe wazi na watakaopatikana na hatia wafikishwe mbele ya vyombo vya sheria. Wanaohusika nao wafanye kazi kwa pamoja na umakini ili kusije kukatoka jambo linaloweza kuathiri mahusiano ya Burundi na hizo nchi zilizotajwa.

Kuna matatizo mengine yanajitokeza hapa tunasema umasikini uliokithiri, mishahara ambayo ipo kwenye kiwango kisicho lingana kwa wafanyakazi wa serikali, ukosefu wa kazi na matatizo ya mashamba yanayotia wasiwasi warundi wote kwa ujumla. Matatizo hayo yanaleta wasiwasi inayoweza kuzusha balaa kwa wananchi wote.

Tukiangalia namna utawala wa CNDD-FDD ulivyoathiri umoja wa kati chama chetu na chama UPD-Zigamibanga, umoja ulioanzishwa wakati tukiwa bado kwenye vita vya uko Mbozi. Ilibidi wanachama waasisi wa vyama hivyo viwili wachukue uamuzi wa kudumisha umoja wao na kuonyesha muelekeo mpya wenye kuleta faraja kwa warundi. Umoja huo ndio utakao kuwa msingi ambao vyama hivyo viwili vitategemea katika kuandaa uchaguzi ujao.

Jambo ambalo mnatakiwa kujua ni kwamba maaandalizi hayo ya uchaguzi ni moja kati ya sababu zilizopelekea wafuasi wa vyama hivyo kunyanyaswa wakianzia kwangu mimi mwenyewe.Kunyanyaswa, kufungwa na kuuwawa kwa baadhi ya wafuasi wa vyama vya upinzani kwa mfano MSD na FNL, hii ni ishara tosha kwamba kuna watawala ambao hawana jambo lingine linalowasumbua zaidi ya kuleta vurugu hapa nchini. Kutokana na sababu hiyo warundi wengi waliona kwamba ni muhimu kusimama kidete na kubadili utawala huu na kuweka utawala unaoheshimu demokrasia.

 • Mabibi na Mabwana,
 • Wanachama wa CNDD-FDD na UPD-Zigamibanga,
Chama CNDD-FDD mlichokua mkifahamu mwaka 2005 sio kilichopo hivi sasa. Chama CNDD-FDD tunachokijua kilibakia bila hitilafu wala kasoro yoyote. Ni kile kilichokubali mkataba wa Arusha na pia kikatia saini kwenye makubaliano ya kusimamisha vita baina ya makundi ya wapiganaji na serikail ya mpito ya Burundi. Hatuwezi kubeba lawama na makosa yaliyofanywa wa watu wengine, maovu hayo yalifanywa na baadhi ya wanachama wenye fikra potofu wanaochukulia chama kama nyezo ya kufanya maovu katika utawala tangu tarehe 7 februari 2007.

Raisi Nkurunziza yupo anakaribia kumaliza awamu ya pili kama kiongozi wa Burundi awamu ambayo ndio ya mwisho kama ilivyoandikwa katika katiba ya nchi, mkataba wa Arusha pamoja na sheria wa chama. Mbinu alizotaka kutumia ili kubadilisha katiba aweze kujichagulisha awamu ya tatu au awamu zingine kama ilivyo kuwa katika ndoto zake zilikua ni kama kupoteza wakati wake kwani warundi walio wengi hawakukubaliani naye.

Ili mambo yaende vizuri, tunamini kwamba wafuasi wetu wakishirikiana pamoja na warundi wote, wawakilishi wa mashikrika yasiyoya kiserikali na wawakilishi wa madini kukataa kwa sauti moja ukiukaji wa katiba .Warumdi wemgi wameonesha msimamo wao na hilo linatupa faraja.

 • Mabibi na Mabwana,
 • Wanachama wa CNDD-FDD na chama UPD-Zigamibanga
Kwa sababu hizo zilizotajwa hapo juu tumejiunga na kuwa kitu kimoja ili kudai haki zetu na tuweze kujenga taifa lenye nguvu kisiasa na kiuchumi. Ili tufike kwenye lengo hilo inapaswa tuwe huru tufanye liwezekanalo vyombo vya sheria viwe huru na vyenye kutekeleza haki sawa kwa wote, pia vyombo vya habari viwe huru.

Nawaalikeni ili tuwe pamoja kwa ajili ya amani, umoja na maendeleo ya kudumu na kusahau tofauti zetu wa kikabila, kidini na kimikoa ili tuweze kujenga taifa lenye nguzo imara. Ili tufikie lengo inatupasa tuwe wazalendo kwani uzalendo njia ndio pekee unayoweza kututoa mikononi mwa wahalifu wanaotaka kuelekeza nchi gizani; hali tuliomo sasa sio ile tuliyopigania.

Chama CNDD-FDD halisi kilikua kimechukua uamuzi wa kuendesha mapambano ya ukombozi ili kurudisha demokrasia, amani, umoja, haki na kujenga upya Burundi ambapo raia atapata mahitaji yake yote ya kila siku;chakula, kuwasomesha watoto na kuwatibisha bila tatizo.Ilani na sera zetu za kisiasa ambazo zilichaguliwa na kiasi kikubwa cha wananchi mwaka 2005 bado ndizo msingi mkuu tanasimamia katika uchaguzi ujao Burundi.

 • Ndugu wananchi,
Tunakabiliwa na majukumu makubwa. jamii ya kimataifa inaelekeza macho kwetu, inatupasa tufanye kazi kwa juhudi na hekima mpaka tutakapofikia ushindi wakidemokrasia ambao ni motisha kwa wafadhili kuja kuchangia katika maendeleo ya taifa letu.

 • Kwa vyombo vya dola,
Sisi kama wananchi wapenda amani na haki tunawaomba muheshimishe sheria za nchi, mikataba ya kimataifa inayo heshimisha haki wa binadamu, kumbukeni kwamba hayo ni majukumu yenu ya kila siku na hasa katika nyakati hizi za kujiandalia uchaguzi. Uwajibikaji, uzalendo, utu na keheshimu desturi za nchi vinatakiwa kudumu daima.

Epukeni ulaghai wowote unaoweza kuwapelekea kutenda tofauti na majukumu yenu ya kulinda raia kama kufunga watu kinyume na sheria na kuua watu kiholela.

 • Waheshimiwa Mabibi na Mabwana,
 • Mabalozi wanchi mbalimbali na wawakilishi wa mashirika ya kimataifa na yale yasiokuwa ya kiserikali,
Tunatumia nafasi hii kuwashukuruni kwa michango yenu katika maendeleo ya nchi yetu, katika hatua wa uandaji wa uchaguzi mkuu tunaoutarajia na hasa kwa ushujaa mlioonyesha katika kuandaa mazungumzo baina ya wanasiasa na serikali.

Licha ya hayo hakuna mtu anayeweza kusahau kwamba nyinyi ni mashahidi wa kutosha kwa yale yanaojili nchini, katika hii miaka kumi ya utawala uliyopo, serikali ya Peter NKURUNZIZA iliandaa mipango mingi ya maendeleo katika sekta mbalimbali kama ukulima, afya, biashara na mengineyo mengi lakini licha ya mipamgo hiyo kuwepo hakuna utekelezeshaji wowote uliofanya kutowa motisha kwa wafadhili wa Burundi.

Kutofanikiwa kwa mipango hiyo kulisababishwa na makosa ya waliokua wakihusika katika utekelezaji wa mipango hiyo ambao hawakufanya kazi yao kikamilifu na kutofuatisha makubaliano waliokubaliana na wafadhili wa Burundi. Kinachosikitisha zaidi ni utumiaji mbaya wa misaada hiyo tunayopata kitu ambaco husababisha kupungua kwa misaada hiyo na kupelekea hali mbaya kwa wananchi.

 • Waheshimiwa Mabibi na Mabwana,
Moja kati ya majukumu yenu ni kujulisha nchi zenu hali halisi ya yale yanayojiri pale mlipo. Kuhusiana na Burundi kuna mengi ya kusema japo iliandaliwa mipango ya maendeleo wananchi bado wanaishi katika hali mbaya na usalama mdogo. Katika afya na elimu bado mambo si mazuri, bei za usafiri na chakula zinazopanda kila wakati mishahara ya wafanyakazi ikibaki palepale, kitu ambacho kinasababisha mishahara yao kutoweza kukidhi mahitaji yao. Kwa ufupi maisha yamekua magumu na serikali hii imezidiwa.

. Kwa namna yeyote ile tunawahitaji na tunawaombeni muwe watetezi wa nchi yetu katika nchi na mashirika yenu ili tuweze kuepukana na tabu ambazo utwala wa Nkurunziza umetuletea.

 • Kwa mashirika yasiyokua ya kiserikali, vyombo vya habari
Tunawashukuruni kwa kazi nzuri mliofanya ya kupigania haki za wananchi, tunawapongeza kwa jitihada zenu katika vita dhidi ya rushwa, usalama mdogo, unyanyasaji wa raia na mengine mengi yanayowakabili raia wa Burundi.

Tunaona kwamba sasa mnaelewe vizuri kuliko ilivyo kuwa mwaka 2007 jinsi gani wafuasi wa CNDD-FDD walioniunga mkono na mimi mwenyewe tulipo kataa utawala wa kimabavu , unyanyasaji, uvunjaji wa haki za binadamu na baadae kunyanyaswa na vyombo vya sheria. Hali kama hii ndio ilisababisha kufungwa kwangu, wengine kufukuzwa kazi hata wabunge kuondolewa katika viti vyao.

Chama chetu CNDD-FDD kiri haribika baada kupata viongozi wasio heshimu sheria.

Kuondolewa wa wabunge 22 katika awamu ya kwanza ni dalili mbaya na ya ajabu. Tuko tayari kuungana na yeyote yule ambaye yupo tayari kubadilisha hali mbaya hii ya kisiasa, nchi yetu iliyomo kupitia uchaguzi huru unaoheshimu demokrasia, hatuwezi sahau kuwa yameshajitokeza makosa mengi katika zoezi la kuandika wapiga kura. Pia wamekuwa makitumia mbinu wa kutishia amani kwa vingozi wa upinzani na wafuasi wao.

Mungu ibariki Burundi.

Mungu walinde watetezi wa demokrasia Burundi.
Burundi Transparence c'est l'actualité en continue